Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raysmuzik adondosha ngoma ‘YKTVBZ’

E3751794 Raysmuzik Young Copie 1010x673 Raysmuzik adondosha ngoma ‘YKTVBZ’

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki kutoka nchini Lagos Nigeria mwenye makazi yake jijini London mkali wa Afro-fusion, Raysmuzik ameachia ngoma yake ya ‘YKTVBZ’ ambayo amewashirikisha SK Golden Boy na Sarchebaby kutoka kwenye mixtape yake Night Owl.

Ngoma hiyo imefanywa na producer Jaylon ambaye amewahi pia kufanya kazi na Mr. Eazi na PsychoYP, lakini pia ‘YKTVBZ’ imepitia kwenye mikono ya producer Sparkzy, ambaye amechanganya na miondoko ya afrobeats na amapiano ndani yake.

Akizungumzia ‘YKTVBZ’, @raysmuzik amesema ”Wimbo huu ni wa kuburudisha zaidi na kuwafanya watu kuwa na furaha, pongezi kwa Sparkzy kwa kuufanya wimbo huu kuwa levo nyingine.”

‘YKTVBZ’ umepata sapoti kubwa kutoka BBC 1Xtra, Capital Xtra, The FADER and Complex na hivyo, RaysMuzik kuwa miongoni mwa wasanii wanaokuja kwa kasi nchini Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live