Baada ya Mwanamuziki Ray Vanny kutoka hadharani na kudai kwamba aliilipa Label ya WCB kiasi cha TSh. Bilioni 1.3 na kuvunja mkataba wake, Mtayarishaji wa Muziki nchini Zest ameibuka na madai yake ambapo amesema Rayvanny ameshindwa kumlipa hata Elfu 50 ya kazi zote ambazo amewahi kumfanyia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mtayarishaji huyo ambaye aliwahi kuzipika ngoma kadhaa za Rayvanny, amesema “Dogo kalipa 1.3 Bilioni kuondoka Wasafi lakini anashindwa kunilipa hata Elfu 50 ya kazi zote nilizowahi kumrekodi.” aliandika Zest na kuendelea
"Kuna namna Producers tunatakiwa kujitazama tunasindikiza sana watu kwenye utajiri sasa naona ni muda sahihi wa kufwatilia haki zangu zote 2023 nataka malipo ya ngoma zote nilizowahi kutengeneza maana mpaka sasa pesa zinaingia kupitia kazi nilizowahi kuzifanya na sioni kitu"