Mon, 3 Jan 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Rapa kutokea Marekani, Kodak Black, amesema mwaka 2022 anataka kuiondoa laana ya kwenda jela tofauti na miaka mingine.
Kodak Black amesema tangu atimize miaka 14 hajawahi kumaliza mwaka bila kwenda jela na kwa sasa anataka abadili historia hiyo.
Kodak Black ameongeza kwa kusema kwa sasa ameshaachana na mwenendo mbaya wa maisha na nguvu zake zote sasa atazielekeza kwenye muziki.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live