Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

R.Kelly akanusha kuachia Albamu mpya

Robert Kelly R Kelly Mwanamuziki kutoka Marekani, R. Kelly

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya jana mashabiki wa R. Kelly walipigwa na butwaa la furaha baada ya kukutana na Album mpya ‘I Admit’ ya mkali huyo ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30 Jela.

Lakini ni kitendo cha muda tu kwani Kampuni ya Sony Music iliishusha Album hiyo kwenye majukwaa ya Spotify na Apple Music.

Mwanasheria wa Mwanamuziki huyo mkongwe, Jennifer Bonjean amekaririwa na mtandao wa The Hollywood Reporter akisema, Album hiyo ilichiwa bila kuidhinishwa, ni kazi ambayo iliwahi kuibiwa.

Bonjean aliendelea kusema kwamba waliwahi kutoa taarifa polisi kwamba kuna baadhi ya ‘Masters’ za R. Kelly ziliwahi kuibiwa lakini hawakufanya uchunguzi wowote.

“Pindi anakamatwa, kulikuwa na vifaa vya studio ambavyo vilichukuliwa. Masters zake zilipotea. Kwa hiyo ni nani aliyekuwa nazo na nani anafaidika nazo, hatumfahamu.” alisema Mwanasheria wa Kellz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live