Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Professor Jay Hajawahi Kukosea

Prof Jay 1 Professor Jay Hajawahi Kukosea

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

LEGEND wa Hip Hop na Bongo Fleva, Professor Jay ameachia bonge la kitu kinachokwenda kwa jina la Hands Up akiwa na G Nako na bila unafiki mashabiki wake wamekubali kwamba jamaa hachuji na wala hajawahi kukosea kwenye muziki wake.

Mashabiki wake wanasema tangu enzi za Zali la Mentali hadi leo, hata kama hatoi ngoma mara kwa mara, lakini akiachia inakuwa ni gumzo kama ilivyo Hands Up kwa sasa ambapo ameteka vijiwe vya kusikiliza na kutazama muziki mitandaoni.

Mbali na kuburudisha tu, lakini jamaa huyu akiachia ngoma, lazima ndani yake kuna mafunzo f’lani ambayo mtu anaweza kusikiliza hata mbele ya wazazi na zinadumu kwenye masikio ya watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live