Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Producer Yogo Beats aachana na Muziki

Yogo Producee Producer Yogoi Beats aamua kuachana na Game ya Muziki

Mon, 14 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia Ukurasa rasmi wa Mtayarishaji Mkubwa wa Muziki hapa nchini @yogobeats ameweka taarifa ya kutangaza rasmi kuachana na Kazi ambayo anatambulika nayo ya utayarishaji wa muziki

Kupitia Post aliyoweka YOGO, Ameandika kuwa "I QUIT THE GAME, SITAKI TENA MZIKI, F**K THIS GAME" Akisindikiza ujumbe huo ambao upo kwenye maandishi Meupe na meusi kwa caption inayosomeka kuwa - Too Much Hunting

Mastaa tofauti wa muziki wa Bongo Fleva wameshangazwa na taarifa hii na wengi wamemuandikia kuwa aache utani na alichokiandika lakini wapo walioanza kuuliza sababu ya kufanya hivyo ni nin, wapo walioshangzwa na taarifa hii na hata mashabiki wengi wamemiminika kwenye comments wakitaka afute na kuacha kuweka hizo habari

Ikumbukwe Yogo Beats anafanya kazi na mastaa kibao wa Bongo Fleva akiwemo @officialalikiba ambae wamefanya nae kazi Nyingi sana kwa miaka takribani mitatu nyuma akiwa kama msimamizi mkuu wa kazi zake

Chanzo: www.tanzaniaweb.live