Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Producer Cukie Daddy aishusha video ya msanii wa Rayvanny

Mac Voice Producer Cukie Daddy aishusha video ya msanii wa Rayvanny

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa sasa ni mwendelezo wa maproducer wa Bongo Flava kuchukua hatua za kudai hakimiliki zao kupitia project walizo husika kutengeneza.

Hivi karibuni Producer tokea Bongo Records kwa P. Funk Majani, Cukie Daddy aliweka wazi kuzungukwa na uongozi wa Next Level Music baada ya kutengeneza wimbo mpya wa Mac Voice unaoitwa Sikuachi, cha ajabu ni kuwa Sign Tone yake ikatolewa na kuwekwa Sign Tone ya official producer wa NLM, Sound Boy kama ndiye aliye tengeneza wimbo huo.

Cukie alitumia ukurasa wake wa Instagram kuonyesha ni namna gani amekwazika na jambo hilo na baada ya hapo akaamua kupotezea, lakini baadaye producer huyo amerudi tena na kuiondoa project hiyo kwenye YouTube channel ya Mac Voice.

Kwa mujibu wa maelezo yake ni kuwa ameendelea kuchukuliwa poa na NLM akiambiwa maneno kuwa ana utoto mwingi, wakati ile ni haki yake. Kwa upande wa Mac Voice, yeye amekataa kabisa kuongelea ishu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live