Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waanza uchunguzi vifo kwenye tamasha la Travis Scott

Travis Polisi waanza uchunguzi vifo kwenye tamasha la Travis Scott

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: BBC

Polisi nchini Marekani imeanza uchunguzi kufuatia vifo vilivyotokea kwenye tamasha la muziki siku ya Ijumaa.Angalau watu 8 walipoteza maisha na mamia wengine kujeruhiwa kufuatia kusukumana na kukanyagana katika tamasha hilo lililofanyika usiku huko Houston, Texas.Waathirika wengi ni vijana wa umri kati ya miaka 14 na 27.

Taharuki ilitokea baada ya kundi la watu kuanza kusongamana kuelekea mbele ya jukwaa wakati wa tamasha la Travis Scott la Astroworld, maafisa wanaohusika na huduma za dharura wameeleza.

Watu 11 wamepelekwa hospitali kutokana mshtuko wa moyo ,na wengine wanane wamepoteza maisha

Watu 300 walikuwa wakipatikwa matibabu ya majeraha kama ya kukatwa na michubuko waliyopata kwenye tamasha hilo lililohudhuriwa na watu 50,000

Tukio hilo lilitokea Ijumaa saa tatu na robo saa za eneo hilo, Mkuu wa idara ya zima moto ya mjini Houston Samuel Peña alieleza.

''Watu walianza kusukumana mbele ya jukwaa, watu wakaanza Hali hiyo ilipoanza kusababisha majeraha kwa watu, taharuki iliongezeka, alisema Bw. Peña

Waandalizi walisitisha tamasha hilo ilipoonekana kuwa watu wengi walikuwa wameumizwa, lakini idadi kubwa ya walioathirika ilizidi uwezo wa watoa huduma, mkuu wa zimamoto aliongeza.

Mapema siku ya Ijumaa, mamia ya watu walikuwa wamekimbia eneo la tukio, wakiangusha mashine za ukaguzi wa usalama ili kuingia kwenye tamasha, chombo cha habari cha ABC13 kinaripoti.

Siku ya pili na ya mwisho ya tamasha, Jumamosi, imeahirishwa."Hakuna mtu angeweza kufikiri haya," Mkuu wa Idara ya Polisi ya Houston Troy Finner alisema. "Lakini tuko hapa, na nadhani ni muhimu sana kwamba hakuna hata mmoja wetu anayebashiri. Hakuna aliye na majibu yote usiku wa leo."

Astroworld ni hafla ya kila mwaka inayofanyika katika bustani ya NRG tangu mwaka 2018, ingawa ilisitishwa mwaka jana kwa sababu ya janga la Covid-19.

Chanzo: BBC