Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngoma ‘Friday Feeling’ ya Chimano Moto - Video

Video Archive
Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MEMBA wa kundi maarufu la Sauti Sol kutoka Kenya, Chimano ameachia singo yake mpya ya Friday Feeling pamoja na video yake, ikiwa ni maandalizi ya kuachia albamu yake ya Heavy is The Crown, inayotarajiwa kutoka mwanzoni mwa 2022.

Akiuzungumzia wimbo huo, Chimano amesema hii ni mara ya kwanza kwa kuachia wimbo wa peke yake na amejitahidi kuja na ubunifu wa hali ya juu katika wimbo huo ambao mashairi yake yameandikwa kwa kushirikiana na wakali wengine, Don Ngatia na Bensoul huku prodyuza akiwa ni DTX.

Video ya wimbo huo, imejawa na utamaduni wa ‘ballroom’ unaotajwa kuwa utambulisho wa wanachama wa LGBTQ, ukiwa umepambwa na miondoko na uchezaji unaoendana na wanachama wa kundi hilo ikiwa ni mwendelezo wa harakati za msanii huyo kujitangaza kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

“Kutoka hadharani na kufurahia vile ulivyoumbwa haipaswi kuwa kazi ngumu kwa sababu baada tu ya kufanya hivyo, wengi huanza kujisikia aibu mbele ya jamii na kujikuta wakipata madhara.

“Wimbo huu ni maalum kwa ajili ya kujikubali mwenyewe kuanzia mwili wako, nguo zako, marafiki zako na fedha zako ulizozipata kwa taabu. Ni hisia za kuwa huru, jifanyie mwenyewe mambo ya ziada!” amesema.

Ameendelea kueleza kuwa Albamu ya HEAVY IS THE CROWN itakayokuwa na nyimbo saba, ni mwanzo wa safari mpya katika maisha yake, na kueleza kwamba kwa muda mrefu alikuwa akitamani kuwa huru na kuwahamasisha watu wanaofanana naye kutokata tamaa ya maisha kwa sababu ya jinsi walivyoumbwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live