Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Yusuf: Eti Nimerudi Mjini Sishtui?

Yusuff+pic Mzee Yusuf:

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MFALME mwenye Taarab yake Bongo, Mzee Yusuf anasema kuwa, watu wanaomsema kuwa amerudi mjinilakini hashtui, ni wale ambao mashabiki wake wa kweli.

Staa huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Nimerudi Town anasema kuwa, asilimia kubwa ya watu wanaoongea kuhusu kufeli kwake baada ya kutangaza kurudi mjini, siyo mashabiki wake kindakindaki na wala huwa hawafuatilii shoo zake kwa sababu kama wangekuwa wanafanya hivyo wasingekuwa wanaongeaongea.

“Wanasema nimerudi mjini sishtui? Unajua hao watu wanaokesha kunisema kuwa kwa sasa sishtui, mimi wala siwashangai kwa sababu naamini kabisa siyo mashabiki wangu na wala kwenye shoo zangu huwa hawahudhurii kabisa ndio maana wanakuwa na maneno mengi, laiti kama wangekuwa wananifuatilia vizuri, basi wangegundua kuwa mimi ndiye msanii pekee wa Taarab kwa sasa ambaye ninajaza kwenye shoo zangu, sasa sijui wanataka nirudi vipi mjini?” Anahoji Mzee Yusuf ambaye awali alitangaza kuacha muziki na kumtumikia Allah, lakini akarevjea tena

Chanzo: www.tanzaniaweb.live