Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamuziki Sauti Sol, ajihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Chimano (600 X 712) Memba wa Kundi la Sauti Sol, Chimano

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Memba wa kundi la Afro-Pop kutoka nchini Kenya Sauti Sol, Willis Austin Chimano amejitokeza na kukiri kushirikiana na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Tamko la hadharani la Chimano lilikuja alipokuwa akielezea wazo la wimbo wake mpya, Friday Feeling, ambapo aliwashirikisha wanajamii wa LGBT.

"Hakuna kujificha tena," aliviambia vyombo vya habari vya nchini Kenya.

Chimani alisema kwa sasa anaishi ukweli wake na atatumia muziki wake kupinga kauli za kiume zenye sumu, chuki na unafiki.

Chimano hajawahi kujitokeza hadharani kama mpenzi wa jinsia moja ingawa hapo awali aliwahi kuonekana na wapenzi wa kiume.

Tamko hilo la hadharani linaweza kuwa kupiga jeki juhudi za kupigania haki za watu wa jamii ya LGBT nchini Kenya, ambapo mapenzi ya jinsia moja yameharamishwa na yoyote atakayebainika anaweza kukumbwa na adhabu ya kifungo cha hadi miaka 14 jela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live