Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muumin, Ally Choki Wamlilia Leyla

Leyla Muumin, Ally Choki Wamlilia Leyla

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAIMBAJI maarufu wa muziki wa dansi nchini, Muumin Mwinjuma na Ally Choki wameelezea kushtushwa na kifo cha mdau mkubwa wa muziki nchini, Leyla Mguto.

Leyla ambaye ni mke wa mdau mwingine wa muziki, Ramadhan Shaaban ‘Dk. Rama’, alifariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mapema leo, Muumin amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Leyla na kwamba yeye na Choki walikuwa karibu sana na familia ya Dk. Rama.

“Mimi na ndugu yangu Choki, tupo nje ya Dar es Salaam, tunaomba wadau wa muziki tushirikiane katika msiba huu, Dk. Rama ni mwenzetu, Leyla pia ni mwenzetu katika mambo ya muziki,” amesema Muumin.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, bendi ya Africans Stars ‘Twanga Pepeta’ ilirekodi wimbo wa Leyla, utunzi wake Dk. Rama na ulikuwa miongoni mwa moja ya vibao vilivyopendwa.

Kwa mujibu wa Dk. Rama, msiba upo Kinondoni Mkwajuni na maziko yatafanyika kesho Kibada, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live