Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrembo amweka pabaya Travis Scott

Travis Scott Malu ataka Travis Scott amuache afanye kazi zake

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jinamizi limekaa upande wa Travis Scott mwishoni mwa mwaka huu, mambo yamekuwa yakimharibia kila uchwao.

Wiki chache zilizopita watu walipoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tamasha lake, leo limeibuka hili la msanii aliyekuwa chini ya label yake Malu Trevejo kutaka rapa huyo amuachie huru na mikataba waliyoingia wakati anamsaini.

Travis Scott alimsaini Malu Trevejo mapema mwaka huu baada ya kukiona kipaji chake kupitia mtandao wa TikTok. Miezi mitatu baadaye, Malu alitangaza kujitoa kwenye label hiyo (Cactus Jack) na Kutangaza kujiunga na Atlantic Records.

Naona hawakumaliza vyema kimikataba na Cactus Jack ya Travis Scott, leo mrembo huyo ameibuka kupitia insta stories na kudai Travis amuachie huru kimikataba la sivyo ataanika uchafu wake uliojificha nyuma ya pazia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live