Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mr Blue na jicho la kimuziki

Blue Pic Data Msanii wa Bongo Fleva, Khery Sameer Rajab 'Mr Blue'

Mon, 27 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii wa Bongo Fleva, Khery Sameer Rajab 'Mr Blue' amesema hapati shida kuandika nyimbo kutokana na muziki kwake ni maisha, hivyo ni rahisi kupata ujumbe unaoihusu jamii anayoipelekea kazi zake.

Amesema anaishi kwenye jamii inayoshabikia nyimbo zake, hivyo kuna wakati anakutana na matukio yanayomfanya aandike nyimbo zitakazowagusa wahusika moja kwa moja.

"Ninaposema muziki ni maisha ni kitu ambacho nakifanya kila siku, nitaimba, nasikiliza, nayaona matukio yanayofanyika kwenye jamii yapo ya kuburudisha na ambayo yanahitaji elimu". amesema Mr Blue na kuongeza;

"Ndio maana sina presha nafanya kazi kwa kujiamini, kwani najua kila msanii ana jicho lake la kuyatafsiri matukio yaliopo duniani ama kwenye jamii zinazotuzunguka, kisha akaandika nyimbo".

Nje na hilo, amesema anafurahishwa na namna ambavyo chipukizi wanakuja kwa kasi, jambo ka msingi analowashauri wafanye kazi kwa bidii na wasiruhusu kiki zitawale muziki.

"Wapo chipukizi wengi wanaofanya vizuri, ninalotamani kuona kwao kazi zao ziongee sana kuliko kutawaliwa na kiki, mashabiki wanahitaji kupata burudani na elimu kupitia vipaji vyao na siyo maisha yao binafsi kuongelewa zaidi". amesema Mr Blue  

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz