RAPA maarufu Bongo, Awadhi Chami 'Moni Centrozone' amefungukia kuhusu rafiki yake wa muda mrefu, Ibrahim Mandingo 'Country Wizzy' kuondoka katika lebo ya Konde Gang inayomilikiwa na msanii Harmonize.
Moni amesema; "Nilimpigia nikaongea nae baada ya saa 24, nikamwambia kwamba umenishangaza hadi mimi, maana nilionana nae kama siku mbili nyuma, nikamuuliza mipango yake, akaniambia na alivyojisikia.
"Nimekutana nae juzi alikuwa anashuti video yake, nafikiri yupo vizuri, yupo tayari kukutana na changamoto mpya baada ya kumaliza mkataba wake, nafikiri Country Wizzy amefanya sana movement, nafikri ana mipango ya kufungua Clik yake itakuwa kitu kizuri sana," amesema Moni.
Country Wizzy ambaye ni rapa mkali hapa Bongo ameachana na Konde Gang aliyojiunga nayo Septemba 13, 2020 baada ya mkataba wake kumalizia na lebo hiyo na kuamua kwenda kutafuta changamoto nyingine nje ya lebo hiyo kubwa Bongo.