Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mirabaha ya Wasanii Gizani

Kiba Mondiz Mirabaha ya Wasanii Gizani

Thu, 30 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI ilisema itaanza kulipa mirahaba ya kazi za wasanii kuanzia Desemba mwaka huu kupitia makusanyo yatakayopatikana kwenye vyombo vya habari vitakavyotumia kazi zao lakini hadi sasa siku tatu zimesalia mwaka ukatike na mambo ni ZZZZZ, yaani giza nene.

Ubashiri wa wengi ulionesha kuwa, huwenda jambo hili likashindikana kutokana na wasanii wenyewe kugawanyika kwa baadhi kukubali kulipwa na wengine kugoma.

Wasanii hasa chipukizi walipinga makusanyo hayo kwa kusema mpango huo utakuja kuua sanaa ya Bongo kwa sababu vyombo vingi vya habari vitasita kutumia kazi za wasanii kwa kuogopa malipo.

Hebu ukifanikiwa kukutana na msanii yeyote au kama wewe ni msanii na unapitia kwenye ukurasa huu @babutale, @majani187# tuambie umeshalipwa chochote?

Msisahau kuwauliza watu wa serikali mchakato huo umefika wapi au bado uko “mpakani unavuka ng’ambo” maana mwaka ndiyo umeyoyoma tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live