Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Migos waachia albamu yao mpya ‘Culture II’, Drake na Kanye West washiriki

Fri, 26 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Kundi la Migos wameachis albamu yao nyingine baada ya kupita mwaka mmoja tangu walipoachia albamu yao ya mwisho iitwayo ‘Culture’.



Quavo, Offset na Takeoff ambao ndio wasanii wanaounda kundi hilo wameachia albamu yao ya ‘Culture II’ ambayo ndani yake ina ngoma 24.

Katika albamu hiyo Migos wamewakutanisha wasanii kibao akiwemo Drake, Travis Scott, Post Malone, 2 Chainz, 21 Savage na wengine.

Albamu hiyo ambayo kwa sasa imeanza kupatikana kupitia Apple Music imetayarishwa na maproducer kibao akiwemo Quavo, DJ Durel, Metro Boomin, Zaytoven, Cardo, Mike Dean, na Kanye West.

Chanzo: bongo5.com