Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marioo afungukia mjengo wa kifahari 'muziki unalipa'

Marioo Mjengo Marioo afungukia mjengo wa kifahari 'muziki unalipa'

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Marioo akiwa kwenye kipindi cha XXL cha Cloudsfm ametolea ufafanuzi juu ya Video pamoja na picha alizoshare katika ukurasa wake wa instagram akionekana akiwa kwenye Mjengo wa Kifahari.

Mkali huyo amesema, anajivunia kukaa kwenye mjengo huo kwani una hadhi bila kujali kwamba amepanga.

"Ni kweli Muziki unalipa kwa sababu hata kama ni kupanga ile nyumba ni Dola 2000 zaidi ya Tsh.Milioni 4.6 kwa mwezi, unaweza kuona the way tunapata mafanikio Unajua mara nyingi tunakesha Mastudio kwa hiyo inatakiwa tuwe na mazingira mazuri ya kujiegesha, tunafika sehemu tunapumzika vizuri Lakini yote na yote mimi nawashukuru sana kwa sapoti wanayonipatia mwanzo mwisho," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live