Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marafiki waja na fursa kuwaendeleza wasanii kimataifa

WhatsApp Image 2021 10 05 At 3.51.56 AM.jpeg Waandaaji wa Tamasha la Marafiki katika mkutano na Waandishi wa Habari

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mkurugenzi na muanzilishi wa Tamasha la marafiki, Isack Abeneko akishirikiana na Ufaransa wameandaa Tamasha litakalofanyika Jijini Dar es Salaam na Bagamoyo likiwa na uwezo wa kuwajengea wasanii katika maeneo mbali mbali ya sanaa na kuwaendeleza Kimataifa.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam,  amesema tamasha hilo litawakutanisha pamoja wasanii zaidi ya 128 wa ndani na nje, pamoja na wadau na wataalamu mbalimbali wa Sanaa kwa ajili ya kushirikishana uzoefu na maarifa kwa lengo la kuinua Sanaa ya muziki nchini.

Amesema tamasha hilo litafanyika kuanzia Oktoba 7 hadi 9 kwa Dar es Salaam na Oktoba 10 Bagamoyo. Pia kaulimbiu ya tamasha hilo ni ‘Muziki na maendeleo ya kijamii’ ikiwa na dhumuni la kuhamasisha vijana na wanamuziki kutumia muziki kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

“Tamasha la Marafiki pia litakuwa na semina za mafunzo na mjadala wa wazi kwa siku tatu, mambo mbalimbali yatajadiliwa na kutolewa elimu inayohusu namna ya kufuata utaratibu wa biashara ya muziki, utengenezaji wa muziki wenye mzunguko na unaofaa, usimamizi wa msanii na jinsi ya kupata soko la ndani na kimataifa, ili kuwaendeleza wasanii nchini,” amesema Abeneko.

Ameongeza kuwa mjadala wa wazi utakuwa juu ya biashara ya muziki na jinsi ya kuufanya uwe muhimu na utumike ndani ya soko la Tanzania na Afrika Mashariki. 

Aidha tunaamini semina ya mafunzo ya biashra ya muziki ni jambo muhimu kwa wasanii wote, wasimamizi wa Sanaa, waandaaji matamasha na wadau mbalimbali wanaojihusisha na Sanaa.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Sanaa (BASATA) Ibrahimu Ibengwe, ametoa wito kwa Watanzania kuunga mkono jitihada za wadau hao ili kuiwezesha sekta ya sanaa nchini kupiga hatua kimaendeleo, huku akieleza kwamba seriakali iko pamoja nao ili kuhakikisha kilakitu kinaenda kama kilivyopangwa.

Chanzo: ippmedia.com