Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama yake Snoop Dogg afariki

Geskwd8y51ixsljv 1635137724.jpeg Mama yake Snoop Dogg afariki

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: Mirror

Mama mzazi wa Rapper Snoop Dogg aitwae Beverly Tate amefariki akiwa na umri wa miaka 70, chanzo cha kifo chake hakijatajwa lakini imeelezwa kwamba alilazwa Hospitali mwanzoni mwa mwaka huu.

Mama huyu ambae ni Mzaliwa wa McComb Mississippi anatajwa kuwa Mtu aliyempenda Mungu na alikua karibu sana na kanisa na hata Snoop Dogg alilelewa kwenye mazingira ya kanisa alipokuwa mdogo.

Snoop aliwahi kusema Mama yake alikua muungwana na ndiye alimshawishi Snoop kumuomba msamaha Mtangazaji wa TV Gayle King aliyezungumzia kesi ya ubakaji ya Kobe Bryant wakati wa msiba wake mwaka 2020 kitendo kilichomkasirisha Snoop na kupost video akitumia lugha kali na kumkosoaā€¯

Chanzo: Mirror