Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lulu Diva alivyopigania maisha ya mama yake mpaka kifo kilipomchukua

Luludivaapic Data Lulu Diva alivyopigania maisha ya mama yake mpaka kifo kilipomchukua

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Msanii wa Bongofleva Lululu Diva amepatwa msiba wa Mama yaka Mzazi ambale amezikwa leo Mkoani Tanga

Akizungumzia msiba huo, mama mdogo wa Lulu Diva, Hadija Mbwana, amesema mama Lulu  alikutwa na umauti akiwa Hospitali ya Lugalo, walipompeleka kwa ajili ya kuangaliwa afya yake.

Amesema waliamua kumpeleka baada ya kumuona ana kitu kimembana shingoni kama kohozi, lakini walipofika hospitali kadri saa  zilivyozidi kwenda hali yake ilizidi kuwa mbaya hadi kufika hatua ya kuwekwa mashine ya kumsaidia kupumua.

Taarifa hizo zilianza kusaambaa juzi  jioni huku mastaa mbalimbali wakiungana naye katika maombolezo ya msiba huo.

Baadhi ya ni pamoja na Nandy, aliyeandika” Pole lulu mungu akupe nguvu wewe na familia nzima  RIP mama.

Wakati Shilole ameandika ‘Najua uchungu najua unavyojiskia sasa hali hii ni ngumu mno sikia tu kwa mwenzio ila kwa tuliondokewa na Mama zetu tunaelewa hali uliyonayo Luludiva  pole kazi ya Mungu haina mkosa.

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Esterlinah Sanga maarufu kwa jina la Linah, aliandindika” Mungu akutie nguvu

tumuombee Mama apumzike kwa Amani” huku msanii Aslay akiandika “Mungu akupe nguvu kwenye kipindi hiki kigumu unachopitia Luludiva.

Ugonjwa wa mama

Ukiachilia mbali salamu hizo za pole,  Januari mwaka huu, katika mahojiano na Mwananchi, Lulu alielezea kiundani ugonjwa wa mama yake ambao ulimlaza kitandani kwa miaka minane .

“Mama yangu alipata ajali na kuvunjika kiuno alivunjika kiuno miaka minane iliyopita na kusababisha mwili wake kupooza”amesema Lulu.

Alisema pamoja na kuelezwa kuwa mama yake anatakiwa matibabu ya aina gani, hakuwa na fedha za kumtibia.

“Alipatiwa vipimo  Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo gharama za upasuaji wa mgongo ilitakiwa nilipe Sh8 milioni, lakini wakati huo hela hiyo sikuwa nayo”alisema na kuongeza.

“Mungu si Athumani, nilipoingia kwenye muziki nikapata shoo nchini Gabon, nililipwa fedha nyingi na kuibua matumaini ya kumtibia mama yangu, kumbuka kila kazi niliyokuwa nikiifanya nilikuwa ninawaza nipate fedha ya kumtibia mama Lulu”alisema.

“Kwa kuwa nilipata fedha nyingi nikampeleka mama yangu  Hospitali ya Agha Khan ambapo gharama ya matibabu ilikuwa  Sh20,000 milioni nikalipa akafanyiwa upasuaji  na mama yangu alianza kusimama japo alikuwa bado kwenye mazoezi,”alisema Lulu Diva.

Alisema mama yake alipata ahueni na kuanza kusimama,lakini muda mfupi baadaye alirudi tena kitandani na hii ni baada ya kujitonesha akiwa anafanya mazoezi kwa kudondoka bahati mbaya.

“Katika upasuaji ili kumrudisha katika hali ya kawaida aliwekewa kiungo bandia kiunoni, hivyo alipodondoka akiwa anafanya mazoezi kilipinda, na kushindwa  tena kusimama mwenyewe,"anasema Lulu Diva.

Namna alivyompambania

Katika mahojiano hayo  na Mwananchi lililotaka kujua alikuwa akimuhudumiaje mama yake kipindi cha nyuma kabla ya usanii.

Lulu  alisema alianza kumuuguza mama yake tangu  akiwa  kidato cha nne, ambapo alikuwa akifanya kazi kwenye duka la nguo.

Alisema alikuwa akilipwa Sh120,000 fedha ambayo ilikuwa ni ndogo ukilinganisha na majukumu yaliyokuwa yanamkabili, lakini alijitahidi kutoa huduma bora kwa wateja na kupewa  tip za hapa na pale, na pia alikuwa akijinyima ilimradi apate hela ya kumtibu mama yake.

“Kuna watu wakinuiona saa hizi wananiona kama mtu wa bata sana, lakini ukweli ni kwamba nimeishi maisha ya shida hadi ya kulala njaa, ila muziki umeniokoa nashukuru kwa hilo ikiwemo kumuuguza mama yangu kipenzi”alisema.

Alisema alifanya yote hayo kwa kujua yeye ndiyo baba, mama kwa mama yake,”Mama alinizaa mimi peke yangu na baba yangu alifariki miaka mingi iliyopita, hivyo nilijua mama ana mimi na mimi nina mama, alinihitaji na nilimuhitaji zaidi ya sana”.

Amtungia wimbo

Aprili mwaka huu, Lulu katika kuonyesha anavyomkubali mama yake, alimtungia wimbo wa kumpa moyo kwa kipindi cha kuumwa anachopitia na kuupa jina la ‘mama’.

Mama Lulu anatarajiwa kuzikwa leo kijijini kwao Maiyanga Muheza,jijini Tanga.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz