Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Luizer Mbutu autaka Uenyekiti Chamudata, mchuano upo hivi...

Luiza Pic Data Luizer Mbutu

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Luizer Mbutu amekuwa mmoja wa wanachama wa Chama cha Muziki wa Dansi (Chamudata) na mwanamke pekee aliyejitokeza kutaka nafasi ya Uenyekiti wa chama hiko.

Hilo limebainika leo Ijumaa Machi 25, 2025 kupitia Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hiko, Faza Lusozi alipozungumza na Mwananchi.

Lusozi amesema katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Aprili 27, 2022, huku nafasi zinazogombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu na wajumbe.

Katika nafasi ya uenyekiti, amesema wanachama sita wamejitokeza, ukiacha Luizer, yupo mwanamuziki wa siku nyingi Hamza Kalala, Joseph Mugire, Mwinjuma Muumin, Said Kaunga na Francis Kaguna.

“Wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti waliojitokeza ni Ramadhani Kitenge, Juma Mbizo na Abdallah Hemba.

“Huku nafasi ya Katibu, yupo Hassan Msumari ambaye anatetea nafasi yake hiyo na Said Kibiriti ambaye ni msemaji wa bendi ya Msondo Ngoma na nafasi ya Katibu Msaidizi wapo Baraka Sulus na Aziz Idd,” amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wa nafasi za ya ujumbe, amebainisha kuwa wamejitokeza watu 13, kati yao yupo Said Mdoe, Bennovilla Mashali, Shomari Kupawa, Tabu Mambosasa, Bernedict Sanga, Matei Lusegei na Gabriel Bakilana.

Wengine ni Cecy Lugome, Andrew Mwampashi, Rhobi Chacha, Sholinda Mwezimpya, Ramadhani Mtuli na Abbu Abubakar.

Hata hivyo nafasi ya Mwekahazina na mwekahazina Msaidi imekosa watu baada ya kukosekana walio na sifa, ambapo moja wapo ni kuwa umesomea kazi hiyo.

Akizungumza nia ya kutaka nafasi hiyo, Luizer amesema ukiacha mbali katiba ya chama chao kumruhusu kutokana na kuwa mwanachama, anataka kupigania haki na maslahi ya wasanii wa dansi ambayo yamekuwa kilio cha muda mrefu.

“Nimefanya kazi muda mrefu kwenye muziki wa dansi hivyo najua changamoto zao ndani nje, naamini nikiwa Mwenyekiti, nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuwapigania haki zao,” amesema Luizer.

Luizer mbali ya kuwa mwimbaji wa Twanga Pepeta, pia ni mtunzi na amefanya kazi na bendi hiyo mwaka wa 23 sasa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz