Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leopard Poemz: Nakula Sahani Moja na Zuchu

Ongeza AUDIO Njdkbeh Leopard Poemz: Nakula Sahani Moja Na Zuchu

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii anayefanya poa kwa sasa kunako anga la muziki mtamu wa Bongo Fleva, Pard Luhanga almaarufu ‘Leopard Poemz amefunguka jinsi ambavyo ameamua kula sahani moja na mrembo anayemzimia kwenye gemu ambaye pia ni msanii mwenzake, Zuhura Othman ‘Zuchu’.

Miongoni mwa stori zinazovuma kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na wawili hao kuachia ngoma za Amapiano kwa pamoja ambapo ngoma ya Leopard inakwenda kwa jina la Siachi Pombe huku ya bibie Zuchu ikiwa inakwenda kwa jina la Kitu.

Leopard anasema kuwa, anafurahi kuona kwamba kila siku anazidi kukua kwenye tasnia ya muziki wa Bongo na kwamba mwakani anataka kufanya makubwa zaidi.

“Kwanza kabisa nafuraha kuona mashabiki wangu wanapokea kile ambacho nakifanya, ngoma yangu ya Siachi Pombe kwa sasa inapatikana kwenye platforms zote na inakimbiza vya kutosha.

“Ninawaahidi mashabiki wangu kwamba 2022 utakuwa mwaka wa kufanya maajabu,” anasema Leopard.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live