Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Koffi Olomide anusurika kwenda Jela, aamriwa kulipa faini, walalamikaji hawajaridhika

Koffi Ngwasuma Antoine Agbepa Mumba "Koffi Olomide"

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya rufaa nchini Ufaransa, imemuondolea mwanamuziki Koffi Olomidé (65)kosa la unyanayasaji wa kingono, lakini ikamtia hatiani kwa kuwashikilia wanawake bila hiari yao.

Mahakama ilibatilisha uamuzi wa 2019 uliompata na hatia ya ubakaji wa mmoja wa wmadensa wake alipokuwa na umri wa miaka 15.

Lakini alipatikana na hatia ya kuwanyima wanawake uhuru wao kwa kuwashiukilia katika jumba la kifahari huko Paris, Ufaransa kati ya 2002 na 2006.

Atatumikia kifungo cha miezi 18, kilichoahirishwa kwa muda na kuwalipa fidia.

Mwendesha mashtaka ya umma alikuwa amependekeza ahukumiwe kifungo cha chini ya miaka minane.

Walalamikaji katika kesi hii "bila shaka hawakuridhishwa na hukumu ya unyanyasaji wa kingono kwa sababi kwa hili lilikuwa kitu cha muhimu zaidi ", alisema wakili David Desgranges ambaye alikuwa akiwawakilisha wanawake hao.

Mmoja wao alikuwa amedai kuwa aliwaingilia kimwili "katika mahoteli, wakati mwingine ndani ya gari na katika studio za kurekodi muziki".

Hata hivyo mahakama iligundua kuwa kitendo chake dhidi ya wanawake hao "kiliwanyima uhuru kwa kuwekwa chini ya uangalizi wa mara kwa mara " na washirika wake wawili ambao waliwazuilia kwenye chumba wakiwa wamefungwa nyuso zao.

Mbali na adhabu ya kifungo ambayo imesimamishwa, nguli huyo ameamriwa kulipa faini Shillingi za Kitanzania Milioni 25-82 kwa kila mcheza shoo wake.

Olomidé, ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba, ni mmoja wa wanamuziki maarufu zaidi barani Afrika.

Olomide mara kadhaa ameshawahi kuingia matatani na mamlaka za kisheria katika nchi mbali mbali kama vile;

Mwaka 2018 Zambia iliamuru kukamatwa kwake baada ya kudaiwa kumshambulia mpiga picha.

Mwaka 2016 alikamatwa na kurejeshwa njumbani baaada ya kuwashambulia wacheza densi wake nchini Kenya.

Mwaka 2012 alipatikana na hatia nchini DR Congo kwa kosa la kumshambulia mtayarishaji wake na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela.

Mwaka 2008 alituhumiwa kwa kumpiga teke mpiga picha wa kituo cha televisheni cha kibinafsi cha RTGA nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini baadaye wawili hao walipatana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live