Baada ya stori na video kusambaa mitandaoni zikionyesha shoo ya KMsanii wa Bongo Fleva, Baba Levo kubuma kule Kigoma huku watu waliohudhuria wakiwa wachache tofauti na ambavyo ilitarajiwa, msanii huyo amemkatia simu mtangazaji aliyetaka kufahamu undani wa suala hilo.
Baada ya stori na video kusambaa mitandaoni zikionyesha shoo ya KMsanii wa Bongo Fleva, Baba Levo kubuma kule Kigoma huku watu waliohudhuria wakiwa wachache tofauti na ambavyo ilitarajiwa, msanii huyo amemkatia simu mtangazaji aliyetaka kufahamu undani wa suala hilo. Ikumbukwe kuwa, Baba Levo amekuwa miongoni mwa wasanii wanaoponda shows za wasanii wenzao wanazofanya kuwa hazijazi watu, hivyo ilitarajiwa show yake ingekuwa ya kinyama sana na pengine ingefunika kuliko zile za wasanii anaowaponda lakini hali ilikuwa tofauti.