Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kayumba, Frida Amani huwaambii kitu kwa Samia

2a2b71b38841fd789c082ba87245b6b3 mwanamuziki wa ku-rap, Frida Amani

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Kayumba Juma na Frida Amani wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyojali sekta ya sanaa na utamaduni.

Wasanii hao walimpongeza Rais Samia kwa nyakati tofauti walipopanda jukwaani kutumbuiza katika hafla ya kuipongeza timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars, Ikulu, Dar es Salaam juzi.

Alianza Kayumba kuimba wimbo wake wa I love you mama na kuwataka waalikwa wote kuimba pamoja naye kama ishara ya kukubali kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

“Naomba nikiimba mpokee ‘I love you mama’ kwa kutambua jitihada za Rais wetu Samia ambaye ameonesha jitihada kubwa katika kuendeleza sanaa na utamaduni maana licha ya kuwa Rais, anavaa umama na kuonesha kuguswa na sisi sote,” alisema Kayumba ambaye ni mshindi wa BSS mwaka 2015.

Naye Frida ambaye aliimba wimbo wa hip hop wa ‘Madame President’ alisema Rais Samia amewafanya wanawake wengi kujiamini ndio maana hata yeye anaimba hip hop ambayo ilionekana kufanywa na wasanii wa kiume pekee.

“Mama ametufanya wanawake wenzake kujiamini ndio maana hata mimi leo naimba hip hop ambayo zamani ilionekana muziki mgumu unaoweza kuimbwa na wanaume pekee,” alisema Frida.

Chanzo: www.habarileo.co.tz