Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanye West, Drake kumbe fresh tu

Kanye Vs Drake (600 X 609) Kanye West amaliza tofauti na Drake

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye wasanii nyota wakubwa duniani Rapa “Ye” maarufu kama Kanye West na Drake wamaliza tofauti zao na sasa hivi mambo ni safi.

Siku chache zilizopita Kanye West alimtumia Drake mualiko wa kuperfom pamoja Los Angeles, tarehe 7 Desemba, mwaka huu huku akimsisitiza pia wamalize tofauti zao kwa lengo la kumsaidia Larry Hoover atoke jela.

Usiku wa kuamkia leo Drake pamoja na Kanye West wameonekana wakiwa pamoja huko Toronto kwenye Party.

Na baadaye wawili hao wali-share picha pamoja na video kwenye mtandao wa instagram wakiwa pamoja.

Hatua hii kubwa na nzuri imewafurahisha wengi na kwa sasa watu wanasubiria kuona perfomance ya aina yake itakayoangushwa huko Los Angeles, Desemba mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live