Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KR Mullah afiwa na baba yake

55844acd2df99708e560c4f5be4e27e4 Rashid Ziada ‘KR Mullah’

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Rashid Ziada ‘KR Mullah’ amefiwa na baba yake mzazi mkoani Lindi.

Taarifa ya kifo cha mzazi wa msanii huyo, kimeelezwa na msanii mwingine wa muziki wa kizazi kipya, Amani Temba ‘Temba’, kupitia ukurasa wake wa instagram leo.

"Pole sana KR Mullah TMK kwa kuondokewa na baba yako mzazi, Mzee Ziada, hakika kazi ya Mungu haina makosa,” ameandika Mheshimiwa Temba, ambaye pamoja na KR Mullah walitamba na kundi la TMK Wanaume Familiy.

Kwa mujibu wa Temba, msiba huo ulitokea usiku wa kuamkia leo mkoani Lindi na kuwa taratibu nyingine za mazishi zitatolewa leo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz