Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jux kugawa Kitita kwa shabiki

IMG 20220228 WA0012 CEO wa African Boy, Jux

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: dar24.com

Jux ametangaza kutoa zawadi kwa shabiki yake atakayeweza kubashiri siku na muda atakaoachia wimbo wake mpya ‘I love you’ alioshirikiana na nyota kutoka nchini Ghana Gyakie.

Kupitia kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram Jux amesema kuwa atatoa zawadi ya shilingi Laki moja ikiwa atajitokeza shabiki atakayepatia chemsha bongo hiyo.

“My amazing fans, Wiki ijayo nina jambo lenu nalileta mjini. Tanzania X Ghana, Video yangu ya wimbo wangu na Gyakie I LoveYou iko tayari, Itatoka wiki ijayo, Ninachohitaji kutoka kwako ni kuniambia hiyo video nitaitoa lini na saa ngapi?.

Ukipatia siku husika na saa ya kutoka video ya #ILoveYou utafurahia, nina zawadi yako ndogo ya Shillingi Laki moja, let’s get busy my people.” Ameandika.

Chanzo: dar24.com