Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jux, Vanessa Mdee uso kwa uso tuzo za Afrimma

70336 Pic+jux

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati habari ya kuachana kwa wasanii Vanessa Mdee na Jux, zikiwa bado za moto, wawili hao kukutana uso kwa uso kwenye tuzo za Afrimma.

Katika tuzo hizo zinazowashirikisha wasanii mbalimbali kutoka nchi za barani Afrika, Jux anawania katika kipengele cha msanii bora wa kiume Afrika Mashariki, huku Vanessa akiwania kipengele cha msanii bora wa kike katika ukanda huo.

Wawili hao watakutana kwa mara ya kwanza tangu watangaze rasmi kuachana na huku Jux akiwa tayari amemtambulisha mpenzi wake mpya aitwaye, Nayika.

Baada ya uamuzi huo wa Jux, Vanessa  alithibitisha kuachana kwao.

Tuzo zitakazowakutanisha zitafanyika  Novemba, 2019 huko Texas, Marekani.

Chanzo: mwananchi.co.tz