Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Justine Bieber kuileta ziara yake Barani Afrika.

Bieber Justin Bieber

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa sasa ni wazi kuwa Afrika linazidi kuwavutia watu wengi kutoka nje, fursa za kibiashara kwa upande wa burudani nazo zimeanza kufunguka kwa wawekezaji na hata wafanyabiashara wa muziki kuanza kuyaingiza baadhi ya mataifa kwenye orodha ya mipango yao.

Mwanamuziki Justin Bieber ameamua kuileta ziara yake ya ‘Justice World Tour’ Barani Afrika katika mji wa Cape Town huko Afrika ya Kusini, tukio linalotarajiwa kufanyika itakapofika September 28 mwaka 2022.

Takribani siku mbili zilizopita Justine Bieber aliweka wazi orodha ya mataifa na miji ambayo ziara yake hiyo itapita kwa kipindi cha mwaka mzima hadi ifikapo mwezi Machi, mwaka 2023.

Kwa kuanzia, Afrika Kusini ndio taifa pekee barani Afrika ambalo ziara hiyo itapita ikiwa imepangwa kuanza rasmi Mei 14, 2020. Japokuwa ililazimika kuahirishwa takribani mara mbili kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 kuendelea kusambaa nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live