Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Justine Beiber apooza uso, afuta matamasha yake yote

Justine Beiber Jusine Bieber, akubwa na ugonjwa wa ajabu

Sat, 11 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki wa Pop duniani kutoka Canada anayefanya shughuli zake za muziki nchini Marekani, Justin Bieber amefuta matamasha yake kadhaa aliyokuwa amepanga kuyafanya kutokana na kukumbwa na tatizo la kupooza uso wake (facial paralysi).

Imeelezwa kuwa nyota huyo amepooza uso wake upande wote wa kulia baada ya kupata virusi wanaoambukiza ugongwa huo kitaalam huitwa Ramsey Hunt Syndrome.

Bieber mwenye umri wa miaka 28 baada ya kupimwa alikutwa na tatizo hilo linaloathiri sehemu kubwa ya mishipa ya fahamu (nerves) za kichwa.

Staa huyo ambaye alikuwa na tour yake aliyoipa jina la Justice Tour huko America ya Kaskazini, tayari ameshafuta tamasha lake la Toronto, Washington DC na New York.

Kupitia video ya dakika 3 aliyoposti mtandaoni, Bieber amesema: “Ni kutokana na kirusi huyu ambaye ameshambulia mishipa yangu ya fahamu (nerves) za sikio na uso, amesababisha uso wangu kupooza.

"Kama unavyoona, siwezi kuchezesha jicho (kukonyeza), siwezi kutabasamu, kwenye huu upande uliopooza. Pua haiwezi kucheza, kwa hiyo kuna kupooza moja kwa moja (full paralysis) kwenye uso wangu.

Bieber ameonekana akijaribu kutabasamu, kuchezesha pua, kukonyeza lakini baadhi ya sehemu za uso wake zimeonekana kutofanya kazi kabisa. Amesema kwa sasa anaendelea na mazoezi ya uso kuhakikisha anarejea katika hali yake ya kawaida.

Albamu yake ya mwisho ya Justice aliiachia mwezi Machi 2021, na imethibitishwa kama platinum Marekani na kushika nafasi ya pili kwenye chati ya Albamu nchini Uingereza. Tour yake ya Amerika Kaskazini inatarajiwa kutamatika Julai mwaka huu.

“Kwa wale mliokwazika kwa kufutwa kwa matamasha yangu ninawaomba radhi sana, siko sawa na sitoweza kufanya matamasha hayo. Hili ni tatizo siriazi,"alisema Bieber.

“Natambua mnaelewa, na nitatumia muda huu kupumzika na kurejea kwenye hali yangu kwa asilimia 100 ili niweze kufanya tena kile ambacho nimeletwa duniani kukifanya. Ila kwa muda huu mfupi sitoweza, ninamwamini Mungu atanisaidia," alisema Bieber.

Ikumbukwe kuwa, mwezi Machi mwaka huu, mke wa staa huyo aitwaye Hailey Bieber, alipelekwa hospitali baada ya kupatwa na tatizo la damu kuganda kwenye ubongo wake, lakini baadae qlisema qlikuwa na stroke iliyosabqbisha kufanyiwa upasuaji kuziba tundu lililokuwa kwenye moyo wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live