Mwanamuziki mahiri kutoka tasnia ya Bongo fleva Jay Melody amevunja ukimya kwa kuweka wazi mambo yanayomkera na yamekuwa yakifanywa na baadhi ya wasanii wa Tanzania.
Nyota huyo mmliki wa ‘Sugar’ moja ya rekodi zinazofanya vizuri kwa sasa nchini, amekemea vikali tabia ya baadhi ya wasanii kujivisha mamlaka ya kuwa madalali wa kazi za wasanii wenzao inapotokea kuna fursa ya kazi inayopitia mikononi mwao.
“Kuna hii tabia ya baadhi ya wasanii mbaya sana, yaani msanii anakupigia msanii mwenzie, Mzee kuna show wana wanakuhitaji labda Kigoma, na wewe una mwambia sawa kaka wape mawasiliano yangu niongee nao.
Kaka mkubwa anajiacha anaanza kukwambia, kwani wewe unafanya show shilingi ngapi niongee nao, hapo ndio kuna tatizo, sasa uongee nao wewe umekuwa Manager wangu umekuwa nani ?. Tufanyeni kazi bhana hiyo tabia ni ya kishamba” ameandika Jay Melody.
Mwimbaji huyo ameutuma ujumbe huo kupitia ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram ‘Insta Story’ akidhihirisha kukwazwa na aina ya vitendo ya namna hiyo, ambavyo kwa madai yake vimekuwa vikifanya na wasanii wenzie.
Jay Melody kwa sasa bado anashikilia nafasi za juu akiwa miongoni mwa wasanii wenye rekodi zenye kufanya vizuri kwenye kiwanda cha muziki Afrika mashari huku wimbo wake ‘Sugar’ ukifikisha jumla ya streams Milioni 1 kwenye mtandao wa Boomplay na jumla ya watazamaji Milion 3.8 kwenye YouTube ndani ya kipindi cha miezi miwili pekee.