Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hili hapa balaa la Mondi

8174e3c6b8674f09dea210fb11ca6312 Dimond Platnumz

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva nchini Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz', ametangaza kuonesha wasanii wa Afrika Mashariki mwaka huu watafanya vizuri zaidi kuliko miaka iliyopita.

Kutokana na hali hiyo amesema tayari amefanya video ya nyimbo zote 10 kwenye albamu yake fupi (EP) ya First Of All (FOA).

“Natamani niwambie kitu kimoja, EP ina video zote 10, video zake ni kali sana, video zake zimekaa, hatucheki na mtu, yote ni kuonesha kwamba wana Afrika Mashariki tupo vizuri,” amesema Diamond.

Ukiachilia rekodi mbalimbali alizowahi kuweka Diamond, hii ni ya kipekee, ambapo ameingiza kwenye trending nyimbo zake zote 10 zilizopo kwenye EP hiyo.

Diamond aliachia rasmi EP hiyo Machi 11, 2022 ikiwa na nyimbo 10 na mpaka sasa imefikisha streams zaidi ya milioni 30 kwenye mitandao tofauti ya kusikilizia muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live