Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya Koffi Olomidé kujulikana leo

Koffi Nguli wa Muziki wa Rhumba Barani Afrika, Koffi Olomide alievaa Barakoa

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji nguli wa mtindo wa Rumba kutoka DRC, Koffi Olomidé, atafahamu hatma ya kesi yake Jumatatu hii, Desemba 13 alasiri.

Mahakama ya Rufaa ya mjini Versailles itatoa uamuzi wake katika kesi ya mashtaka ya unyanyasaji wa kingono dhidi yake. Upande wa mashtaka uliomba, Oktoba mwaka jana, kifungo cha miaka minane jela dhidi ya msanii huyo.

Bado haihafahamika iwapo Koffi Olomide atakuwepo mahakamani kujua kinashomsubiri, Jumatatu hii, Desemba 13 mchana huko Versailles. Mawakili wake wanasema kuwa mteja wao hana hatia na wana imani kwamba atafutiwa mashitaka.

Aliposikilizwa, mwezi Oktoba mwaka huu, Koffi Olomidé alikosoa "uongo" kutoka upande wa mashitaka. "Hizi ni tuhuma zisizokuwa na msingi," "njama" za "kutaka kuharibu kazi (yangu)", alisema.

Mwimbaji huyo alikuwa akijibu shutuma za wanawake wanne kutoka DRC, kati ya wacheza densi wake wa zamani ambao waliwasilisha malalamiko kati ya mwaka 2007 na 2013. Wanamtuhumu kwa kuwafungia kwenye banda lenye ulinzi karibu na Paris, wakati alipokuwa akitembelea Ufaransa, na kuwalazimisha kufanya naye mapenzi, bila ridhaa yao. Koffi Olomidé alijitetea vikali na kukanusha tuhuma zote.

Akiwa na umri wa miaka 65, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kujieleza hadharani kuhusu mashtaka dhidi yake. Hakuwa amehudhuria kesi yake ya kwanza mnamo mwaka 2019 mbele ya Mahakama ya Jinai ya Nanterre, ambapo alikuwa amehukumiwa katika mahakama ya mwanzo kifungo cha miaka miwili jela kwa "unyanyasaji wa kingono" kwa mmoja wa wasichana hawa, aliyechukuliwa kuwa alikuwa hajatimiza umri wa kufanya mapenzi wakati wa tukio hilo- na kuachiliwa kufutia mashtaka mengine dhidi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live