Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize na maigizo ya mrembo wa Kibrazil

Harmo Lover (600 X 469) Harmonize na tetesi za penzi jipya

Sat, 13 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Flava, Harmonize au Konde Boy ameonyesha ishara ya kama ameingia katika uhusiano mpya wa kimapenzi na mwanamke mwingine, lakini kuna utata kuhusu mrembo huo.

Hii ni baada ya kupumzika kwa miezi michache tangu alipoachana na Mwigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja.

Kupitia InstaStori yake usiku wa kuamkia leo alipost picha ikimuonyesha yeye pamoja na mwanamke wa Kizungu na kuandika maneno yanayo maanisha kuwa hiyo ni kumbukumbu, na dakika chache zilizopita amepost tena maandishi yanayosomeka kuwa hatimaye amepata mpenzi wa maisha yake.

Ikumbukwe kuwa Harmonize ameshawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi yaliyozaa ndoa na Sarah kabla ya kuvunjika na kuanzisha uhusiano na Kajala.

Lakini swali tata ni kuwa katika picha hizo mbili ambazo amepost Harmonize kuna jina la Ilary Duarte.

Katika ukurasa wa Instagram jina hilo la Ilary Duarte linamuonyesha mrembo kutoka Brazil ambaye anaonekana ni mtu wa kuremba.

Hadi sasa haijajulikana uhusiano wa jina hilo la Ilary Duarte kutumika katika picha za Harmonize na kile alichokionyesha kuhusu mpenzi wake mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live