Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize kutoa nyimbo mfululizo

46cd860682e1343e8d216b525acafbd8.jpeg harmonize

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amesema mwaka 2022 atawashangaza wengi kwa kutoa nyimbo mfululizo, ambazo zingine zake na zingine atakuwa ameshirikishwa.

Akifafanua zaidi kwa mwaka 2022 tayari ameingia katika nyimbo zaidi ya tano, ambapo ipo nyimbo ya Niwewe aliyoshirikishwa na Killy, Serious ambaye yupo peke yake, wimbo wa Championi alioshirikishwa na mwanamuziki Fik Fameica na wimbo wa Woman.

Alisema hizo ni sehemu ya nyimbo, ambazo zinaendelea kutoka kwa mwaka huu, huku lengo likiwa kutoa nyimbo nyingi zaidi huku pia akiunga mkono juu ya kazi, ambazo wamekuwa wakitoa wasanii wake kutoka lengo ya Konge Gang.

Miongoni mwa msanii ambaye anatoka katika lebo yake ni Killy, ambaye anatarajia kutoa albamu fupi ‘Ep’ yenye nyimbo tano, liyomshirikisha Christian Bella na Ibra.

Chanzo: www.habarileo.co.tz