Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Nitawashangaza Watu Wengi 2022

Harmo Kijiji Harmonize

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSANII mkubwa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul almaarufu Harmonize au Konde Boy Mjeshi anasema kuwa, mwaka huu wa 2022 atawashangaza wengi kwa kile atakachokifanya.

Harmonize anasema kuwa, amepanga kuufanya muziki wa Bongo Fleva upenye na watu waupokee kimataifa, lakini amegundua lugha ni tatizo kwani watu hawajui wanaimba nini kwa sababu asilimia kubwa ya wasikilizaji wa muziki huo duniani wanazungumza Kingereza.

Akizungumza wakati wa sherehe ya usikilizaji wa albam yake mpya ya High School uliofanyika ndani ya Pam Village, Mikocheni jijini Dar, Konde Boy anasema kama ni kutangaza lugha ya Kiswahili wamefanya, lakini wanahitaji kubadilika na kushindana na soko la kimataifa.

“Leo wasanii wa Nigeria wanaonekana wanafanya vizuri kwa sababu wanaimba kwa lugha ambayo inazungumzwa duniani na muziki wao unapokelewa haraka tofauti na sisi, tunahitaji kuimba nyimbo kwa lugha ya kigeni kupata mashabiki wengi na hicho ndicho nitakachokifanya na kitawashangaza wengi mwaka huu (2022),” anasema Konde Boy na kusisitiza kuwa amepanga kuachia albam ambayo itakuwa ni ya Kingereza tupu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live