Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize: Lugha inatukwamisha

E3e6393011515f87eca50cb32aca7764.jpeg Rajabu Abdul, Harmonize

Sun, 2 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amesema lugha ni kikwazo cha muziki wa Tanzania kushindwa kufanya vizuri kimataifa.

Akizungumza Dar es Salaam juzi alisema muziki unapenya na watu wanaupokea lakini hawajui wanaimba nini kwa sababu asimilia kubwa ya mashabiki duniani wanazungumza Kiingereza.

Alisema kama ni kutangaza lugha ya Kiswahili wamefanya, lakini wanahitaji kubadilika na kushindana na soko la kimataifa.

“Leo wasanii wa Nigeria wanaonekana wanafanya vizuri kwa sababu wanaimba kwa lugha ambayo inazungumzwa duniani na muziki wao unapokelewa haraka tofauti na sisi, tunahitaji kuimba nyimbo kwa lugha ya kigeni kupata mashabiki wengi,” alisema.

Harmonize alisema muziki wa bongo ni mzuri kwa hiyo ukibadilishwa na kuimba kwa lugha za kigeni unaweza kufanya vizuri na kwenda sambamba na wa Nigeria.

“Sanaa imekua lakini muziki bado, tumekuwa tunakuza lugha lakini unapopenya wenzetu hawaelewi tunahitaji kuwaelewesha ni kitu gani tunaimba, ni muda wa kueneza muziki wetu, la sivyo tutakimbia lakini kuvuka daraja tutashindwa,” alisema.

Alisema amefanya utafiti na kugundua katika nyimbo zake alizoimba kwa kuchanganya lugha ndizo zenye watazamaji wengi kuliko zile alizoimba kwa lugha ya Kiswahili pekee.

Kiongozi huyo kutoka lebo ya Konde Gang ni miongoni mwa wasanii ambao wamekuwa wakiimba nyimbo nyingi kwa kuchanganya lugha. kama Bedroom, High school iliyobeba albamu yake, Outside, Mang’dakiwe Remix, What do you miss na nyingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live