Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

G- Nako Aachia Mini-tape Mpya ya ‘Kitimoto’

GNAKO Gnako

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa kizazi kipya, G-Nako ‘Warawara’ kutoka Kundi la Weusi lenye maskani yake jijini Arusha, ameachia Mini-Tape yake aliyoipa jina la Kitimoto, ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wake katika kuelekea kuumaliza mwaka 2021.

Akiizungumzia mini-tape hiyo ambayo inajumuisha ngoma 9 ndani yake ambayo ameiachia kupitia Jukwaa la Boomplay, G- Nako amesema imesheheni ngoma kali ambazo zitawaburudisha mashabiki zake zikiwemo ‘Unakaaje Chini’, ‘Stimu’, ‘Poison’ aliyomshirikisha Country Wizzy na ‘Shika Shila’ aliomshirikisha Young Lunya.

Nyingine ni ‘Acha Dharau’, ‘Booty Goo’ aliowashirkisha Spicy Meg na Petra, ‘Loko Loko’, ‘Ooh Mama’ pamoja na ‘Kitoko’ ambapo amesema mtu yeyote atakapoanza kusikiliza wimbo wa kwanza, hatatamani uishe mpaka nyimbo zote zitakapoisha.

Kuhusu jina la mini-tape hiyo, G-Nako amesema Kitimoto ni kifupisho cha Kiti cha Moto, akimaanisha kwamba mtu akianza kusikiliza ngoma zilizopo kwenye mini-tape hiyo, hawezi kukaa kutokana na ukali wa ngoma zilizopo ndani yake.

Kuachiwa kwa mini-tape hiyo inakuwa ni ujio mpya wa mkali huyo ambaye jina lake halisi ni George Mdemu, baada ya miezi tisa kupita bila ya kuachia kazi zake mwenyewe kama solo artist tangu aachie wimbo wake wa mwisho ambao ni ‘Jiachie’ uliotoka Machi 4, 2021.

G-Nako ni miongoni mwa marapa wachache Tanzania ambao wamekuwa na unyumbulifu (flexibility) mkubwa katika sanaa ya muziki kutokana kujaaliwa uwezo wa kuimba pamoja na ku-rap.

Minitape hiyo kwa sasa inapatikana Boomplay pekee mpaka Jumapili na unaweza kuisikiliza kupitia mtandao wa Boomplay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live