Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Future auza haki ya nyimbo zake kwa mabilioni ya pesa

Future Rocket Ship Future auza haki ya nyimbo zake kwa mabilioni ya pesa

Thu, 22 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa maarufu kutoka nchini Marekani Nayvadius DeMun Wilburn 'Future' ameripotiwa kuuza haki za nyimbo zake za kuanzia mwaka 2004 hadi 2020 kwa Kampuni ya Influence Media Partners.

Tovuti za Variety na Billboard zimeripoti, dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya kuanzia ($65M - $75M) yaani zaidi ya TSh. Bilioni 175.

Catalog iliyouzwa na Future ina Jumla ya nyimbo 612 ikiwemo Kolabo za wakali kama Drake, Kendrick Lamar, Rihanna na The Weeknd.

Mwaka 2022 Kampuni ya Influence Media Partners ilitumia kiasi cha ($300 million) kununua haki za nyimbo za Bruno Mars, Dua Lipa, Ariana Grande na Justin Bieber.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live