Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Foby aomba siku 10 kusikilizwa

Foby S (600 X 748) Msanii wa Bongo Fleva, Foby anatarajiwa kuachia EP yake

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Foby, ameomba apewe siku kumi tu ziwe za kwake ili watu waweze kusikiliza EP yake mpya ambayo anatarajia kuiachia mwezi ujao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter mkali huyo wa ngoma ya "bwana Mkubwa" ameandika:

“Nna ombi kwa wasanii na mashabiki, Naombeni mnipe siku kumi tu za kupromote na kusikiliza EP yangu Wasanii msitoe EP tarehe hizo na mashabiki ipeni sikio EP.

"Siombi kwa kuogopa haitofanya poa La hasha! Naomba ili tushindane na masoko ya nchi zilizotuzidi."

Msanii huyo ameomba siku hizo kuanzia tarehe 2/12 mpaka tarehe 12/10 mwaka huu.

Hivyo ni wakati wa wapenzi wa Foby kukaa mkao wa kula kutoka kwa mkali huyo wa kubembeleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live