Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Foby aachana na Muziki ??

Foby Muda 1 Msanii wa Bongo Fleva, Foby

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ombi lake kwa wadau wa muziki ikiwemo wasanii na mashabiki kutotiliwa maanani, msanii wa muziki wa kizazi kipya Foby amedokeza kuachana na muziki.

Ikumbukwe Novemba, Foby aliwaomba wasanii wenzake wasitoe nyimbo wala EP kuanzia tarehe 2 Desemba mpaka tarehe 12 Desemba na pia aliwaomba wadau wa muziki kuipa sikio Extended Playlist hiyo aliyoipa jina la Me, Myself and I (MMI).

Tofauti na alivyotarajia wasanii waliendelea kutoa nyimbo hivyo akaikosa nafasi aliyoiomba kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Foby ameandika:

“Oiii wanangu hio EP ndio ilikuwa ya mwisho kama zawadi yenu Bye bye Tanzania Music Industry, Thanks for everything God bless you all”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live