Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Drake, Ne-yo, Chriss Brown kwenye album mpya ya Aaliyah

Aaliyah.jfif Aaliyah

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pamoja na kwamba Mziki wa Mwanamziki wa zamani Aaliyah kuingia kwenye huduma za kustream kuna uwezekano wa kutolewa kwa albamu mpya.

Katika mahojiane yake na Billboard Mjomba wa mwanamziki Aaliyah ambaye pia ni mwanzilishi wa studio ya Background Records Barry Hankerson aliweka wazi mpango wake wa kutoa Albam ya Aaliyah kwa kushirikisha wanamziki wengine.

Wakati tarehe ya kutolewa ikiwa inatarajiwa kutangazwa, Hankerson amejikuta anachukua muda mrefu kukamilisha kazi hiyo ambayo inasemekana amewashirikisha wanamziki maarufu kama Drake, Future, Ne-yo, Chriss Brown na snoop dogg.

Wakati huo huo Msanii Timbaland tayari ametoa wimbo wenye maneno yanayotoka kwenye wimbo wa Aaliyah huku Msanii Tank akijitolea kuunga mkono kazi hiyo.

Akizungumzi ujio wa Album hiyo Hankerson amesema "imekuwa ni kazi nzuri sana, shida ni kwamba watu wamenikasirikia sana kwasababu mziki haukuweza kutoka wakati ambao watu wanauhitaji" Hata hivyo nimekubaliana nao sina namna"

Ni miaka 20 sasa tangu afariki mwanamziki Aaliya na Kwa mara ya kwanza nchini Marekani Hatimaye Mziki wa Aaliyah utakuwa kwenye huduma za mziki wa mtandaoni kama sehemu ya kazi za studio ya Background kwa kushirikiana na kampuni inayojitegemea katika usambazaji wa muziki ya Empire.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live