Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diva asusa kula kisa Alikiba

Diva Pic Data Diva asusa kula kisa Alikiba

Fri, 5 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Kelvin KagamboMore by this Author UNAKUMBUKA ule mtiti ulioibuka mwaka jana ambapo aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bawse alikuwa akivujisha meseji anazodai alikuwa anatumiana na staa wa Bongofleva, Alikiba kuthibitisha kuwa wawili hao waliwahi kutoka kimapenzi?

Tena sasa wakati Alikiba akiwa kwenye ndoa na mke wake Amina, sasa hilo sekeseke bado halijatoka kichwani kwa mwanadada huyo ambaye jina lake halisi ni Loveness Malinzi, kwani amefunguka tena kuwa alivyogombana na Alikiba kipindi kile, alijifungia ndani bila kula kwa muda wa wiki nzima.

Diva ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyofanya na chombo kimoja cha habari nchini baada ya kuulizwa kama anaweza kukaa siku mbili bila kula kwa sababu ya kugombana na mpenzi wake.

“Ndiyo. Nilipogombana na Ali nilikaa wiki nzima bila kula. Sipendi kumuongelea sana lakini huo ndiyo ukweli,” alisema.

Licha ya kwamba Alikiba ametajwa mara kadhaa kuwa alikuwa akitoka kimapenzi na Diva, lakini mwenyewe hakuwahi kukiri uhusiano huo na hata Diva alipovujisha meseji zinazodaiwa ni za Kiba, mkali huyo wa wimbo wa Infedele aligoma kuziongelea.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz