Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Zuchu, Marioo, Darasa Watesa Chati za Apple Music

DIAMONJD ZUCHU 1 Zuchu na Rayvanny

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

IKIWA tupo mwishoni mwa mwaka 2021, Kampuni ya muziki ya Apple imetoa chati ya nyimbo 100 bora zaidi kwa mwaka 2021 ambapo kwa upande wa Tanzania mastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zuchu, Marioo na wengineo wameonekana kuteka zaidi chati hiyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo, kuachia chati hiyo ambayo inaangazia nyimbo 100 Bora za 2021; nyimbo za muziki wa mazoezi uliochezwa zaidi kwenye Apple Music na nyimbo bora zilizosikilizwa na na watu wengi zaidi duniani kote.

Chati hizi za kimataifa zinaangazia na kusherehekea mwaka mwingine mzuri katika muziki, na kwa pamoja hutoa mtazamo wa kipekee na wa kimataifa kuhusu muziki mzuri zaidi wa mwaka.

Tazama chati kuu za Apple Music 2021 hapa chini na usikilize orodha kamili za kucheza za chati 100 kwenye Apple Music kwenye kiunganishi hiki: music.apple.com

Katika chati hiyo, kuna orodha ya kategori tofauti tofauti katika nchi mbalimbali duniani zikiwemo Tanzania, Kenya, Nigeria, Ghana na nyingine nyingi.

Mbali na mastaa hao, wengine waliongia kwenye chati hiyo ni pamoja na Rayvanny, Mbosso, Jux na wasanii wengine wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live