Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, The Game mbioni kuachia goma jipya

Image 161.png Diamond, The Game mbioni kuachia goma jipya

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Mwanamuziki maarufu wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ amethibitisha ujio wa wimbo wake mpya aliomshirikisha mwana Hip Hop kutoka nchini Marekani, Jayceon Terrell Taylor maarufu kama ‘The Game’.

Taarifa hiyo imeenea kwa kasi baada ya kuonekana kwa Comment ya nyota huyo kwenye moja ya chapisho la ukurasa wa Instagram wa msanii Diamond platnumz, lililohusu onyesho lake litakalofanyika Kigali nchini Rwanda.

Kwenye chapisho hilo, rapa The Game aliweka comment ya emoji za moto kama kiashiria cha kupendezwa na kazi za Diamond, ambapo muda mfupi baada ya comment hiyo Diamond alijibu kwa kuandika ‘They are not ready for us’ akimaanisha ‘Hawako tayari kwa ajili yetu.

Hata hivyo, kauli hiyo ilitoa kiashiria cha kuwa pengine wawili hao tayari wamekwishafanya kazi ya pamoja au wanatazamia kufanya hivyo siku za usoni.

Miaka ya hivi karibuni, mwanamuziki Diamond amewavutia wasanii wengi wakubwa kutoka mataifa mbali mbali, ikiwamo Marekani ambao wengi wao wamekuwa wakishindwa kuzuia hisia zao juu ya mwimbaji huyo kiasi cha kuweka bayana kuvutiwa naye hata kuamua kumfuata kwenye kurasa zake za mktandao ya kijamii akiwemo rapa P.diddy, na wengineo.

Chanzo: dar24.com