Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Rosa Ree watajwa mara nyingi tuzo Afrima

Diamondpiccc Wasanii waliotajwa tuzo za Afrima

Thu, 23 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Wasanii wa Tanzania , Diamond Platnumz na Rosa Ree wamenga’ara kwenye vipengele vingi katika Tuzo za Muziki Afrika (Afrima) zitazofanyika Novemba mwaka huu nchini Nigeria.

Orodha ya wateule wa tuzo hizo imeanikwa jana Jumatano Septemba 22,2021, ambapo wasanii wengi kutoka Tanzania wakiingia katika vipengele 13, huku Diamond na Rosa Ree wakijitokeza kwenye vingi zaidi ya wengine.

Kwa upande wa Diamond wimbo wa Waah! ndio umembeba, kwani licha ya kumuingiza katika vipengele vinne pia umetajwa katika vipengele saba vikiwemo wimbo bora wa mwaka, video bora ya mwaka, wimbo unaochezeka na wimbo bora wa kushirikiana.

Pia Waah! Umeingia katika vipengele vya msanii bora wa mwaka na msanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

Wimbo huo uliotoka miezi tisa iliyopita mpaka sasa umeshatazamwa zaidi ya mara milioni 85 katika mtandao wa Youtube.

Mbali ya Diamond mwingine aliyejitokeza kwenye vipengele vingi katika tuzo hizo, ni msanii wa muziki wa kufokafoka, Rosa Ree, ambaye ameingia katika vipengele vinne. Advertisement

Vipengele alivyotajwa Rosa Ree na wimbo wake kwenye mabano ni Msanii bora wa kike,Msanii bora wa Hiphop, msanii wa muziki wa Raggae Dancehall(That Girl) na msanii bora wa kike Afrika Mashariki.

Msanii mwingine ni Zuchu ambaye anawania vipengele vitatu kikiwemo cha wimbo wa mwaka kupitia wimbo wa ‘Number One’ aliomshirikisha Rayvanny.

Kipengele kingine ni msanii anayechipukia na msanii bora wa kike Afrika Mashariki ambapo anachuana na Nandy, Spice Diana na Rosaree.

Alikiba pia ameingia katika tuzo hizo akiwania kipengele cha chaguo la watazamaji kupitia wimbo ‘Jelous’ na msanii bora wa kiume Afrika Mashariki akichuana na Diamond, Harmonize,Darasa na Rayavanny.

Dj Sinyorita pia anawania tuzo hizo katika kipengele cha DJ bora, huku mwandaaji wa muziki Laizer akiwania kipengele cha mwandaaji muziki bora wa mwaka na mwongozaji Kenny anawania kipengele cha muongozaji bora wa video wa mwaka kupitia wimbo Waah!.

Tuzo zote za muziki Afrika hufanyika kila mwaka na zilianzishwa na Kamati ya Kimataifa ya AFRIMA, kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika kwa lengo la kutunza na kusherehekea kazi za muziki, talanta na ubunifu kote barani Afrika huku ikitangaza urithi wa kitamaduni wa kiafrika

Chanzo: Mwananchi