Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platnumz, Ruge Mutahaba, Bi Kidude wapewa tuzo ya heshima TMA

Diamonddpic Data Diamond Platnumz

Sun, 3 Apr 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ni miongoni mwa watu waliopewa tuzo za heshima katika utoaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2021.

Tuzo hiyo imetolewa Jumamosi Aprili 2, 2022 katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe katika uwasililishaji wa kazi za wasanii ili kuingia katika ushindani wa tuzo hizo, msanii huyo  hakuwasilisha kazi zake kushindanishwa kwa kile alichoeleza anaangalia zaidi kushindana na wasanii wa nje ya nchi.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi wa Sanaa na Utamaduni kutoka Wizara ya Sanaa na Utamaduni, Dk Emmanuel Ishengoma kwa niaba ya msanii huyo.

Akitangaza sababu ya kumpa Diamond tuzo hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa (Basata), Mtiko Mniko, amesema ni kutokana na kuonyesha kwa vitendo muziki ni biashara, kuuza muziki nje ya Tanzania na kutangaza kiswahili

Ukiacha Diamond wengine waliopewa tuzo hiyo ya heshima ni marehemu Ruge Mutahaba, Bi Kidude na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz