Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Anapenda Kuwa Juu Peke Yake?

Unachezaje Diamond Diamond Anapenda Kuwa Juu Peke Yake?

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MIONGONI mwa mjadala mkali unaoendelea ni juu ya staa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz kudaiwa kupenda kuwa juu peke yake au na timu yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Si tuhuma ngeni kwamba, Diamond au Mondi ni mmoja wa wasanii wenye maringo na tabia ya majivuno na kutopenda maendeleo ya wasanii wengine.

Hata hivyo, mmoja wa watetezi wake ni jamaa ambaye ni msanii aitwaye Lambert ambaye anatoa ya kwake ya moyoni kuhusu uvumi huo kwa kuwaeleza alichokiona baada ya kukutana uso kwa uso na Diamond.

“Acha niwe muwazi hasa kwa wale watu wenye tabia za kuwasemea watu uongo, several times nimesikia watu wakisema Diamond hapendi wasanii wengine na anapenda kuwa juu yeye tu, jambo ambalo nadhani kuna watu wanakubaliana na hilo suala kwa sababu labda hawajawahi kupata nafasi ya kujua ukweli.

“Kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kukutana na Diamond na kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kushiriki jukwaa moja na yeye.

“Lakini kitu kimoja ambacho nitaheshimu milele ni furaha yake kujua kwamba kuna wasanii kama sisi ambao tunaishi nchini Marekani, lakini bado tunapambana kukuza Kiswahili na kufanya muziki tukiwa hukuhuku.

“Hanijui, ila Diamond nikiri alitumia muda wake ambao angefanya mambo mengine ila aliniweka chini na kunishauri mambo mengi sana juu ya sanaa, lakini kubwa zaidi ni kuniambia tuendelee kupambana kuhakikisha Swahili Nation inafika duniani kote.

“Nashangaa msanii kama Diamond ambaye hatujawahi kukutana ila ametumia muda wake kunishauri mambo makubwa kwa faida yangu maneno ya kwamba anaringa sijui anapenda wengine washuke yanatoka wapi.

“My brother once again thanks so much can’t wait kukutana na wewe next time nikija Tanzania na nakuombea watu wazidi kujua thamani na upendo wako kwa watu wengine.

“If you don’t have any nice word to say to someone so don’t force bad to came to you so you can have something to say. Much respect Diamond Plantumz,” anasema Mr Lambert.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live